Genesis 38:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hira akawauliza wenyeji wa Enaimu, “Yuko wapi yule mwanamke kahaba aliyekuwa kando ya njia karibu na hapa?” Wakamjibu, “Hapa hapajawa na mwanamke kahaba.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawauliza watu walioishi mahali pale, “Yuko wapi yule kahaba wa mahali pa ibada za sanamu aliyekuwa kando ya barabara hapa Enaimu?” Wakamjibu, “Hakujawahi kuwa kahaba wa mahali pa ibada za sanamu hapa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akauliza watu wa mahali pale, akisema, Yuko wapi yule kahaba aliyekuwapo Enaimu kando ya njia? Wakasema, Hakuwako hapa kahaba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hira akawauliza wenyeji wa Enaimu, “Yuko wapi yule mwanamke kahaba aliyekuwa kando ya njia karibu na hapa?” Wakamjibu, “Hapa hapajawa na mwanamke kahaba.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawauliza watu wanaoishi mahali pale, “Yuko wapi yule kahaba wa mahali pa kuabudia miungu aliyekuwa kando ya barabara hapa Enaimu?” Wakamjibu, “Hajawahi kuwepo mwanamke ye yote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawauliza watu wanaoishi mahali pale, “Yuko wapi yule kahaba wa mahali pa kuabudia miungu aliyekuwa kando ya barabara hapa Enaimu?” Wakamjibu, “Hajawahi kuwepo mwanamke yeyote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akauliza watu wa mji ule, akisema, Yuko wapi yule kahaba aliyekuwapo Enaimu kando ya njia? Wakasema, Hakuwako hapa kahaba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hira akawauliza wenyeji wa Enaimu, “Yuko wapi yule mwanamke kahaba aliyekuwa kando ya njia karibu na hapa?” Wakamjibu, “Hapa hapajawa na mwanamke kahaba.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alipowauliza watu wa mahali hapo kwamba: Yuko wapi yule mwanamke mgoni wa patakatifu aliyekaa njiani hapo Enaimu? Wakamwambia: Huku hakuwako mwanamke mgoni wa patakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akauliza watu wa mahali pale, akisema, Yuko wapi yule kahaba aliyekuwapo Enaimu kando ya njia? Wakasema, Hakuwako hapa kahaba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hira akauliza wenyeji wa Enaimu: “Yuko wapi yule mwanamuke kahaba aliyekuwa kando ya njia karibu na hapa?” Wakamujibu: “Hapa hapajakuwa mwanamuke kahaba.”