Genesis 38:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya miezi mitatu, Yuda akapata habari, “Tamari, mke wa mwanao amekuwa kahaba, tena amepata mimba kwa kufanya ukahaba.” Basi, Yuda akaamuru, “Mtoeni nje achomwe moto!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya miezi mitatu, Yuda akaambiwa, “Tamari mkweo ana hatia ya kuwa kahaba, na sasa ana mimba.” Yuda akasema, “Mtoeni nje, achomwe moto hadi afe!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya miezi mitatu, Yuda akapata habari, “Tamari, mke wa mwanao amekuwa kahaba, tena amepata mimba kwa kufanya ukahaba.” Basi, Yuda akaamuru, “Mtoeni nje achomwe moto!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya miezi mitatu Yuda akaambiwa, “Tamari mkweo ana hatia ya kuwa kahaba, na matokeo yake ana mimba.” Yuda akasema, “Mtoeni nje na achomwe moto hadi afe!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya miezi mitatu Yuda akaambiwa, “Tamari mkweo ana hatia ya kuwa kahaba, na matokeo yake ana mimba.” Yuda akasema, “Mtoeni nje na achomwe moto hadi afe!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mke wa mwana wako, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya miezi mitatu, Yuda akapata habari, “Tamari, mke wa mwanao amekuwa kahaba, tena amepata mimba kwa kufanya ukahaba.” Basi, Yuda akaamuru, “Mtoeni nje achomwe moto!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miezi mitatu ilipopita, Yuda akapashwa habari kwamba: Mkweo Tamari amefanya ugoni, naye akapata mimba kwa huo ugoni. Ndipo, Yuda aliposema: Mtoeni, ateketezwe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha miezi mitatu, Yuda akapata habari hii: “Tamari, muke wa mwana wako amekuwa kahaba, tena amepata mimba kwa kufanya ukahaba.” Basi, Yuda akaamuru: “Mumutoshe inje achomwe kwa moto!”