Genesis 38:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokuwa wakimtoa nje, Tamari akatuma ujumbe kwa baba mkwe wake, akisema, “Mwenye vitu hivi ndiye aliyenipa mimba. Kwa hiyo, nakuomba umtambue mwenye pete hii na kamba yake, na fimbo hii.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokuwa akitolewa nje, akatuma ujumbe kwa baba mkwe wake kusema, “Nina mimba ya mtu mwenye vitu hivi.” Akaongeza kusema, “Angalia kama utatambua pete hii na kamba yake pamoja na fimbo hii ni vya nani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipotolewa, alipeleka watu kwa mkwewe, akisema, Mimi nimepewa mimba na mtu mwenye vitu hivi. Akasema, Tambua basi, vitu hivi ni vya nani, pete hii, na kamba hii, na fimbo hii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokuwa wakimtoa nje, Tamari akatuma ujumbe kwa baba mkwe wake, akisema, “Mwenye vitu hivi ndiye aliyenipa mimba. Kwa hiyo, nakuomba umtambue mwenye pete hii na kamba yake, na fimbo hii.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipokuwa akitolewa nje, akatuma ujumbe kwa baba mkwe wake kusema, “Nina mimba ya mtu mwenye vitu hivi.” Akaongeza kusema, “Angalia kama utatambua kwamba pete hii na kamba yake pamoja na fimbo hii ni vya nani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokuwa akitolewa nje, akatuma ujumbe kwa baba mkwe wake kusema, “Nina mimba ya mtu mwenye vitu hivi.” Akaongeza kusema, “Angalia kama utatambua kwamba pete hii na kamba yake pamoja na fimbo hii ni vya nani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipotolewa, alituma watu kwa mkwewe, akisema, Mimi nimepewa mimba na mtu mwenye vitu hivi. Akasema, Tambua basi, vitu hivi ni vya nani, pete hii, na kamba hii, na fimbo hii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokuwa wakimtoa nje, Tamari akatuma ujumbe kwa baba mkwe wake, akisema, “Mwenye vitu hivi ndiye aliyenipa mimba. Kwa hiyo, nakuomba umtambue mwenye pete hii na kamba yake, na fimbo hii.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipotolewwa akatuma kwa mkwewe kwamba: Mimi nimepata mimba kwake yeye aliye mwenye vitu hivi; akaendelea kusema: Mtambue mwenye pete hii yenye muhuri na mwenye mshipi huu na mwenye fimbo hii!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipotolewa, alipeleka watu kwa mkwewe, akisema, Mimi nimepewa mimba na mtu mwenye vitu hivi. Akasema, Tambua basi, vitu hivi ni vya nani, pete hii, na kamba hii, na fimbo hii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokuwa wakimutoa inje, Tamari akatuma ujumbe kwa baba mukwe wake, akisema: “Mwenye vitu hivi ndiye aliyenipa mimba. Kwa hiyo, ninakuomba umutambue mwenye pete hii na kamba yake, na fimbo hii.”