Genesis 38:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Onani alijua kwamba hao watoto wasingekuwa wake. Kwa hiyo, alipolala na mke wa nduguye, alimwaga chini mbegu ya uzazi, asije akampatia nduguye watoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga mbegu chini ili asimpatie ndugu yake uzao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Onani alijua kwamba hao watoto wasingekuwa wake. Kwa hiyo, alipolala na mke wa nduguye, alimwaga chini mbegu ya uzazi, asije akampatia nduguye watoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga chini mbegu za kiume ili asimpatie ndugu yake uzao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga chini mbegu za kiume ili asimpatie ndugu yake uzao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, alimwaga mbegu chini asimpe nduguye uzao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Onani alijua kwamba hao watoto wasingekuwa wake. Kwa hiyo, alipolala na mke wa nduguye, alimwaga chini mbegu ya uzazi, asije akampatia nduguye watoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuwa Onani alijua, ya kama huyo mzao hatakuwa wake yeye, basi, kila mara alipoingia kwa mkewe kaka yake kwanza akaziangusha mbegu zake chini, asimpatie kaka yake uzao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Onani alijua kwamba hao watoto hawangekuwa wake. Kwa hiyo, alipolala na muke wa ndugu yake, alimwanga chini mbegu ya uzazi, kusudi asimupatie ndugu yake watoto.