Genesis 39:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yosefu alipochukuliwa mpaka Misri, Mmisri mmoja aitwaye Potifa ambaye alikuwa ofisa wa Farao na mkuu wa kikosi chake cha ulinzi, akamnunua kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huu Yusufu alikuwa amechukuliwa hadi Misri. Mmisri aliyeitwa Potifa, mmoja wa maafisa wa Farao, na aliyekuwa mkuu wa walinzi, akamnunua Yusufu kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yosefu alipochukuliwa mpaka Misri, Mmisri mmoja aitwaye Potifa ambaye alikuwa ofisa wa Farao na mkuu wa kikosi chake cha ulinzi, akamnunua kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huu Yosefu alikuwa amechukuliwa mpaka Misri. Mmisri aliyeitwa Potifa aliyekuwa mmojawapo wa maafisa wa Farao, mkuu wa ulinzi, akamnunua Yosefu kutoka kwa Waishimaeli waliomleta Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huu Yusufu alikuwa amechukuliwa mpaka Misri. Mmisri aliyeitwa Potifa aliyekuwa mmojawapo wa maafisa wa Farao, mkuu wa ulinzi, akamnunua Yusufu kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri, naye Potifa, ofisa wa Farao, mkuu wa askari walinzi, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yosefu alipochukuliwa mpaka Misri, Mmisri mmoja aitwaye Potifa ambaye alikuwa ofisa wa Farao na mkuu wa kikosi chake cha ulinzi, akamnunua kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yosefu alipopelekwa Misri, Potifari aliyekuwa mtumishi wa nyumbani mwa Farao na mkuu wao waliomlinda Farao akamnunua mikononi mwao wale Waisimaeli waliompeleka huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yosefu aliposhushwa kwenda mpaka Misri, Mumisri mumoja anayeitwa Potifari ambaye alikuwa jemadari wa mufalme wa Misri na mukubwa wa waaskari walinzi, akamununua kutoka kwa Waisimaeli waliomuleta Misri.