Genesis 39:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, bwana wake Yosefu alipoyasikia maneno ya mkewe, kwamba ndivyo mtumishi wake alivyomtendea, akawaka hasira,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Potifa aliposikia kisa alichosimuliwa na mkewe, akisema, “Hivi ndivyo mtumwa wako alivyonitenda,” hasira yake ikawaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya mkewe aliyomwambia, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, bwana wake Yosefu alipoyasikia maneno ya mkewe, kwamba ndivyo mtumishi wake alivyomtendea, akawaka hasira,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Potifa aliposikia kisa hiki mkewe alichomweleza, akisema, “Hivi ndivyo mtumwa wako alivyonitenda.” Hasira ya Potifa ikawaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Potifa aliposikia kisa hiki mkewe alichomweleza, akisema, “Hivi ndivyo mtumwa wako alivyonitenda.” Hasira ya Potifa ikawaka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa bwana wake aliposikia maneno aliyoambia na mkewe, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, bwana wake Yosefu alipoyasikia maneno ya mkewe, kwamba ndivyo mtumishi wake alivyomtendea, akawaka hasira,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, bwana wake alipoyasikia haya maneno ya mkewe, aliyomwambia ya kwamba: Mtumwa wako amenifanyia haya na haya, akakasirika na kuwaka moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya mkewe aliyomwambia, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, bwana wa Yosefu aliposikia maneno ya muke wake, kwamba ndivyo mutumishi wake alivyomutendea, akawaka hasira.