Genesis 39:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo mkuu wa gereza alimweka Yosefu awe mkuu wa wafungwa wote humo gerezani; kila kitu kilichofanyika humo kilifanywa kwa mamlaka yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo msimamizi wa gereza akamweka Yusufu awe mkuu wa wafungwa pamoja na kusimamia yote ambayo yalitendeka mle gerezani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo mkuu wa gereza alimweka Yosefu awe mkuu wa wafungwa wote humo gerezani; kila kitu kilichofanyika humo kilifanywa kwa mamlaka yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo msimamizi wa gereza akamweka Yosefu awe mkuu wa wafungwa pamoja na kusimamia yote ambayo yalitendeka mle gerezani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo msimamizi wa gereza akamweka Yusufu awe mkuu wa wafungwa pamoja na kusimamia yote ambayo yalitendeka mle gerezani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliokuwemo gerezani; na yote yaliyofanywa humo, yeye ndiye aliyeyafanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo mkuu wa gereza alimweka Yosefu awe mkuu wa wafungwa wote humo gerezani; kila kitu kilichofanyika humo kilifanywa kwa mamlaka yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu mkuu wa kifungo akatia mkononi mwa Yosefu wafungwa wote waliokuwamo mle kifungoni, yote waliyoyafanya humo yawe kazi yake yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo mukubwa wa kifungo akamuweka Yosefu akuwe mukubwa wa wafungwa wote mule katika kifungo. Kila kitu kilichofanyika mule kilifanywa kwa mamlaka yake.