Genesis 39:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo mkuu wa gereza hakujishughulisha tena na kitu chochote alichokabidhiwa Yosefu kwa maana Mwenyezi-Mungu alikuwa pamoja na Yosefu na kufanikisha kila kitu alichofanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msimamizi wa gereza hakujishughulisha tena na kitu chochote kilichokuwa chini ya uangalizi wa Yusufu, kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja na Yusufu, akimfanikisha kwa kila alichofanya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala mkuu wa gereza hakuangalia neno lililoko mkononi mwa Yusufu; kwa kuwa Bwana alikuwa pamoja naye. Bwana akayafanikisha yote aliyoyafanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo mkuu wa gereza hakujishughulisha tena na kitu chochote alichokabidhiwa Yosefu kwa maana Mwenyezi-Mungu alikuwa pamoja na Yosefu na kufanikisha kila kitu alichofanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msimamizi wa gereza hakujishughulisha tena na kitu cho chote kilichokuwa chini ya uangalizi wa Yosefu, kwa sababu BWANA alikuwa pamoja na Yosefu akimfanikisha kwa kila alichofanya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msimamizi wa gereza hakujishughulisha tena na kitu chochote kilichokuwa chini ya uangalizi wa Yusufu, kwa sababu bwana alikuwa pamoja na Yusufu akimfanikisha kwa kila alichofanya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala mkuu wa gereza hakufuatilia kazi iliyokuwa mikononi mwa Yusufu; kwa kuwa BWANA alikuwa pamoja naye. BWANA akayafanikisha yote aliyoyafanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo mkuu wa gereza hakujishughulisha tena na kitu chochote alichokabidhiwa Yosefu kwa maana Mwenyezi-Mungu alikuwa pamoja na Yosefu na kufanikisha kila kitu alichofanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika yote, mkuu a kifungo aliyoyatia mkononi mwake, hakikuwamo cho chote, alichokitazama mwenyewe, kwa kuwa Bwana alikuwa na Yosefu, nayo yote aliyoyafanya Bwana akayafanikisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala mkuu wa gereza hakuangalia neno lililoko mkononi mwa Yusufu; kwa kuwa BWANA alikuwa pamoja naye. BWANA akayafanikisha yote aliyoyafanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mukubwa wa kifungo hakujishugulisha tena na kitu chochote Yosefu alichopewa kwa maana Yawe alikuwa pamoja na Yosefu na kufanikisha kila kitu alichofanya.