Genesis 39:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tokea wakati Potifa alipomfanya Yosefu kuwa msimamizi wa nyumba yake na mwangalizi wa mali yake, Mwenyezi-Mungu akaibariki nyumba ya huyo Mmisri kwa ajili ya Yosefu. Baraka za Mwenyezi-Mungu zikawa juu ya kila alichokuwa nacho, nyumbani na shambani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuanzia wakati huo Potifa alipomweka Yusufu kuwa msimamizi wa nyumba na mali yake yote aliyokuwa nayo, Mwenyezi Mungu aliibariki nyumba ya Mmisri huyo kwa sababu ya Yusufu. Baraka ya Mwenyezi Mungu ilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa, nyumbani na shambani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tokea wakati Potifa alipomfanya Yosefu kuwa msimamizi wa nyumba yake na mwangalizi wa mali yake, Mwenyezi-Mungu akaibariki nyumba ya huyo Mmisri kwa ajili ya Yosefu. Baraka za Mwenyezi-Mungu zikawa juu ya kila alichokuwa nacho, nyumbani na shambani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuanzia wakati huo Potifa alipomweka Yosefu kuwa msimamizi wa nyumba na mali zake zote alizokuwa nazo, BWANA aliibariki nyumba ya Potifa kwa sababu ya Yosefu. Baraka ya BWANA ilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa, nyumbani na shambani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuanzia wakati huo Potifa alipomweka Yusufu kuwa msimamizi wa nyumba na mali zake zote alizokuwa nazo, bwana aliibariki nyumba ya Mmisri huyo kwa sababu ya Yusufu. Baraka ya bwana ilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa, nyumbani na shambani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa tokea wakati alipomweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Baraka za BWANA zikawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tokea wakati Potifa alipomfanya Yosefu kuwa msimamizi wa nyumba yake na mwangalizi wa mali yake, Mwenyezi-Mungu akaibariki nyumba ya huyo Mmisri kwa ajili ya Yosefu. Baraka za Mwenyezi-Mungu zikawa juu ya kila alichokuwa nacho, nyumbani na shambani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tangu hapo, alipomweka nyumbani mwake kuyasimamia yote, aliyokuwa nayo, Bwana akaibariki nyumba ya huyu Mmisri kwa ajili yake Yosefu; mbaraka ya Bwana ikayakalia yote yaliyokuwa yake nyumbani na shambani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa BWANA ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tokea wakati Potifari alipomufanya Yosefu kuwa musimamizi wa nyumba yake na mwangalizi wa mali yake, Yawe akabariki nyumba ya yule Mumisri kwa ajili ya Yosefu. Baraka za Yawe zikakuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho, ndani ya nyumba na katika shamba.