Genesis 39:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu hiyo Potifa alimpa Yosefu mamlaka juu ya mambo yake yote, naye Potifa akaacha kushughulika na chochote isipokuwa tu chakula chake mwenyewe. Yosefu alikuwa kijana mzuri na wa kupendeza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Potifa akamwachia Yusufu uangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho. Yusufu alipokuwa msimamizi wa mali yake, Potifa hakujishughulisha na kitu chochote isipokuwa chakula alichokula. Yusufu alikuwa mwenye umbo zuri na sura ya kuvutia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu hiyo Potifa alimpa Yosefu mamlaka juu ya mambo yake yote, naye Potifa akaacha kushughulika na chochote isipokuwa tu chakula chake mwenyewe. Yosefu alikuwa kijana mzuri na wa kupendeza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Potifa akamwachia Yosefu uangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho, Yosefu alipokuwa katika uongozi, Potifa hakuwa na sababu ya kujishughulisha na kitu cho chote isipokuwa chakula alichokula. Yosefu alikuwa mwenye umbo zuri na sura ya kuvutia;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Potifa akamwachia Yusufu uangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho, Yusufu alipokuwa katika uongozi, Potifa hakuwa na sababu ya kujishughulisha na kitu chochote isipokuwa chakula alichokula. Yusufu alikuwa mwenye umbo zuri na sura ya kuvutia;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu chochote chake, ila hicho chakula alichokula tu. Naye Yusufu alikuwa mtu mzuri, na mwenye uso mzuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu hiyo Potifa alimpa Yosefu mamlaka juu ya mambo yake yote, naye Potifa akaacha kushughulika na chochote isipokuwa tu chakula chake mwenyewe. Yosefu alikuwa kijana mzuri na wa kupendeza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo akamwachia Yosefu yote, aliyokuwa nayo, yawe mkononi mwake, naye mwenyewe hakujua chake cho chote, isipokuwa chakula chake, alichokila. Naye Yosefu alikuwa mzuri wa umbo na wa uso.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu. Naye Yusufu alikuwa mtu mzuri, na mwenye uso mzuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hiyo Potifari alimupa Yosefu mamlaka juu ya mambo yake yote, naye Potifari akaacha kushugulika na chochote isipokuwa tu chakula chake mwenyewe. Yosefu alikuwa kijana muzuri na wa kupendeza.