Genesis 39:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yosefu akakataa na kumwambia huyo bwana wake, “Kamwe! Bwana wangu amenipa mamlaka juu ya kila kitu hapa nyumbani na, kwa vile niko, hajishughulishi na kitu chochote tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Yusufu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa msimamizi, bwana wangu hajishughulishi na kitu chochote katika nyumba hii; kila kitu alicho nacho amenikabidhi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yosefu akakataa na kumwambia huyo bwana wake, “Kamwe! Bwana wangu amenipa mamlaka juu ya kila kitu hapa nyumbani na, kwa vile niko, hajishughulishi na kitu chochote tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Yosefu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa katika uongozi, bwana wangu hahusiki na kitu cho chote katika nyumba hii, kila kitu alicho nacho amenikabidhi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Yusufu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa katika uongozi, bwana wangu hahusiki na kitu chochote katika nyumba hii, kila kitu alicho nacho amenikabidhi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yosefu akakataa na kumwambia huyo bwana wake, “Kamwe! Bwana wangu amenipa mamlaka juu ya kila kitu hapa nyumbani na, kwa vile niko, hajishughulishi na kitu chochote tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akakataa, akamwambia mkewe bwana wake: Tazama! Bwana wangu hajui cho chote kilichomo humu nyumbani, ninachokiangalia, nayo yote, aliyo nayo, ameyatia mkononi mwangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yosefu akakataa na kumwambia yule muke wa bwana wake: “Sikiliza! Bwana wangu amenipa mamlaka juu ya kila kitu hapa ndani ya nyumba na hajishugulishi na kitu chochote tena.