Genesis 4:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Leo umenifukuza kutoka ardhi yenye rutuba na mbali nawe. Basi, nitakuwa mtu wa kutangatanga, asiye na makao maalumu duniani, na yeyote atakayeniona ataniua.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga duniani bila utulivu, na yeyote anionaye ataniua.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Leo umenifukuza kutoka ardhi yenye rutuba na mbali nawe. Basi, nitakuwa mtu wa kutangatanga, asiye na makao maalumu duniani, na yeyote atakayeniona ataniua.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Leo unanifukuza kutoka katika nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na ye yote anionaye ataniua.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na makao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Leo umenifukuza kutoka ardhi yenye rutuba na mbali nawe. Basi, nitakuwa mtu wa kutangatanga, asiye na makao maalumu duniani, na yeyote atakayeniona ataniua.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, umenifukuza leo hivi katika nchi hii, nami nitajificha, nisiuone uso wako tena, niwe mwenye kukimbiakimbia na kutangatanga katika nchi hii, kisha atakayeniona ataniua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Angalia, leo umenifukuza kutoka udongo wenye mboleo na mbali nawe. Basi, nitakuwa mukimbizi na mwenye kutangatanga katika dunia, na yeyote atakayeniona ataniua.”