Genesis 4:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Sivyo! Atakayekuua wewe Kaini atalipizwa mara saba.” Basi, Mwenyezi-Mungu akamtia Kaini alama ya tahadhari, ili yeyote atakayemwona asimuue.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia, “La, sivyo! Ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini, atalipizwa kisasi mara saba.” Kisha Mwenyezi Mungu akamwekea Kaini alama ili yeyote angemwona asimuue.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Sivyo! Atakayekuua wewe Kaini atalipizwa mara saba.” Basi, Mwenyezi-Mungu akamtia Kaini alama ya tahadhari, ili yeyote atakayemwona asimuue.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini BWANA akamwambia, “La sivyo, ikiwa mtu ye yote atamwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi.” Kisha BWANA akamwekea Kaini alama ili mtu ye yote ambaye angemwona asimwue.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini bwana akamwambia, “La sivyo, ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi.” Kisha bwana akamwekea Kaini alama ili mtu yeyote ambaye angemwona asimuue.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Sivyo! Atakayekuua wewe Kaini atalipizwa mara saba.” Basi, Mwenyezi-Mungu akamtia Kaini alama ya tahadhari, ili yeyote atakayemwona asimuue.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Bwana akamwambia: Atakayemwua Kaini atalipizwa mra saba. Kisha Bwana akamtia Kaini alama, kila atakayemwona asimwue.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yawe akamujibu: “Hapana, sivyo! Atakayekuua wewe Kaina atalipizwa mara saba.” Basi, Yawe akamutia Kaina kitambulisho hata yeyote atakayemwona asimwue.