Genesis 4:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sila naye alimzaa Tubal-kaini, ambaye alikuwa mhunzi wa vyombo vyote vya shaba na chuma. Dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini, ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake Tubal-kaini alikuwa Naama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sila naye alimzaa Tubal-kaini, ambaye alikuwa mhunzi wa vyombo vyote vya shaba na chuma. Dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sila naye alimzaa Tubal-kaini, ambaye alikuwa mhunzi wa vyombo vyote vya shaba na chuma. Dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sila naye akamzaa Tubalkaini, naye alikuwa mhunzi aliyejua kufua vyombo vyote vya shaba na vya chuma; naye umbu lake Tubalkaini alikuwa Nama.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake Tubal-kaini alikuwa Naama.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Sila akazaa Tubali-Kaina, ambaye alikuwa mufuaji wa vyombo vyote vya shaba na chuma. Dada ya Tubali-Kaina alikuwa Nama.