Genesis 4:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila sikieni sauti yangu! Sikilizeni nisemayo enyi wake za Lameki. Mimi niliua mtu kwa kunijeruhi, naam, nilimuua kijana kwa kuniumiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila, nisikilizeni mimi; wake wa Lameki sikieni maneno yangu. Nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana mdogo kwa kuniumiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila sikieni sauti yangu! Sikilizeni nisemayo enyi wake za Lameki. Mimi niliua mtu kwa kunijeruhi, naam, nilimuua kijana kwa kuniumiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila nisikilizeni mimi; wake wa Lameki sikieni maneno yangu. Nimemwua mtu kwa kunijeruhi, kijana mdogo kwa kuniumiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila nisikilizeni mimi; wake wa Lameki sikieni maneno yangu. Nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana mdogo kwa kuniumiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni ninachosema; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila sikieni sauti yangu! Sikilizeni nisemayo enyi wake za Lameki. Mimi niliua mtu kwa kunijeruhi, naam, nilimuua kijana kwa kuniumiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lameki akawaambia wakeze Ada na Sila: Isikieni sauti yangu, ninyi wakeze Lameki! Yategeni masikio yenu, myasikie maneno yangu! Nimeua mtu, kwani aliniumiza, naye ni kijana, lakini alinitia mavilio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lameki akawaambia wake zake: “Ada na Sila musikie sauti yangu! Musikilize maneno ninayosema enyi wake za Lameki. Maana niliua mutu kwa sababu ya kunipiga, nilimwua kijana kwa kuniumiza.