Genesis 40:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati fulani baada ya mambo hayo, maofisa wawili wa mfalme wa Misri walimkosea mfalme. Maofisa hao walikuwa mtunza vinywaji mkuu na mwoka mikate mkuu wa mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya muda, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosa bwana wao, mfalme wa Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati fulani baada ya mambo hayo, maofisa wawili wa mfalme wa Misri walimkosea mfalme. Maofisa hao walikuwa mtunza vinywaji mkuu na mwoka mikate mkuu wa mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya muda, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya muda, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati fulani baada ya mambo hayo, maofisa wawili wa mfalme wa Misri walimkosea mfalme. Maofisa hao walikuwa mtunza vinywaji mkuu na mwoka mikate mkuu wa mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, mambo hayo yalipomalizika, mkuu wa watunza vinywaji vya mfalme wa Misri na mkuu wa wachoma mikate wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosa bwana wao, mfalme wa Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati fulani nyuma ya mambo hayo, wakubwa wawili waliomutumikia mufalme wa Misri wakamukosea. Wakubwa wale walikuwa mutunza vinywaji mukubwa na mupishi mukubwa wa mukate wa mufalme.