Genesis 40:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya siku tatu Farao atakunyanyua kutoka gerezani na kukurudisha tena katika cheo chako. Utaweza tena kumpa Farao kikombe mkononi kama ulivyokuwa unafanya hapo awali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya siku tatu, Farao atakutoa gerezani na kukurudisha kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mkononi mwake, jinsi ulivyofanya ulipokuwa mnyweshaji wake awali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya siku tatu Farao atakunyanyua kutoka gerezani na kukurudisha tena katika cheo chako. Utaweza tena kumpa Farao kikombe mkononi kama ulivyokuwa unafanya hapo awali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku hizi tatu, Farao atakutoa gerezani na kukuweka tena kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mikononi mwake, kama vile ulivyokuwa unafanya ulipokuwa mnyweshaji wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku hizi tatu, Farao atakutoa gerezani na kukuweka tena kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mikononi mwake, kama vile ulivyokuwa unafanya ulipokuwa mnyweshaji wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya siku tatu Farao atakunyanyua kutoka gerezani na kukurudisha tena katika cheo chako. Utaweza tena kumpa Farao kikombe mkononi kama ulivyokuwa unafanya hapo awali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
siku tatu zitakapopita, Farao atakupa kukiinua kichwa chako, kwani atakurudisha katika kazi yako, umpe kikombe chake Farao mkononi mwake, kama ilivyokupasa kale, ulipokuwa mtunza vinywaji vyake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya siku tatu mufalme atakunyanyua kutoka katika kifungo na kukurudisha tena katika cheo chako. Utaweza tena kumupa mufalme kikombe kwa mukono kama ulivyokuwa unafanya pale mbele.