Genesis 40:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika ungo wa juu, kulikuwa na vyakula mbalimbali vilivyookwa kwa ajili ya Farao. Lakini, ndege walikuwa wakivila kutoka ungo huo kichwani pangu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika kikapu cha juu kulikuwa na aina zote za vyakula vilivyookwa kwa ajili ya Farao, lakini ndege walikuwa wakivila kutoka kikapu nilichobeba kichwani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika ungo wa juu, kulikuwa na vyakula mbalimbali vilivyookwa kwa ajili ya Farao. Lakini, ndege walikuwa wakivila kutoka ungo huo kichwani pangu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika kikapu cha juu kulikuwa na aina zote za vyakula vilivyookwa kwa ajili ya Farao, lakini ndege walikuwa wakivila kutoka kwenye kikapu nilichokuwa nimebeba kichwani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika kikapu cha juu kulikuwa na aina zote za vyakula vilivyookwa kwa ajili ya Farao, lakini ndege walikuwa wakivila kutoka kwenye kikapu nilichokuwa nimebeba kichwani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika ungo wa juu, kulikuwa na vyakula mbalimbali vilivyookwa kwa ajili ya Farao. Lakini, ndege walikuwa wakivila kutoka ungo huo kichwani pangu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo katika ungo wa juu vilikuwamo vikate vizuri vyo vyote vya Farao, wachoma mikate wanavyovitengeneza, nao ndege wakavila mwenye ungo kichwani pangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika kitunga cha juu, kulikuwa aina mbalimbali za mikate kwa ajili ya mufalme. Lakini, ndege walikuwa wakikula kutoka kitunga kile juu ya kichwa changu!”