Genesis 40:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo siku ya tatu, ambayo ilikuwa siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake, Farao aliwaandalia karamu watumishi wake wote. Akawatoa gerezani mtunza vinywaji wake mkuu na mwoka mikate mkuu, akawaweka mbele ya maofisa wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya tatu ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo siku ya tatu, ambayo ilikuwa siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake, Farao aliwaandalia karamu watumishi wake wote. Akawatoa gerezani mtunza vinywaji wake mkuu na mwoka mikate mkuu, akawaweka mbele ya maofisa wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mnamo siku ya tatu, ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mnamo siku ya tatu, ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo siku ya tatu, ambayo ilikuwa siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake, Farao aliwaandalia karamu watumishi wake wote. Akawatoa gerezani mtunza vinywaji wake mkuu na mwoka mikate mkuu, akawaweka mbele ya maofisa wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya tatu ikawa siku ya kuzaliwa kwake Farao; ndipo, alipowaandalia watumishi wake wote karamu; hapo katikati ya watumishi wake akampa mkuu wa watunza vinywaji naye mkuu wa wachoma mikate kuviinua vichwa vyao,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ilipotimia siku ya tatu, ambayo ilikuwa siku ya kufanya sikukuu ya kuzaliwa kwake, mufalme wa Misri akafanyia watumishi wake wote karamu. Akatoa katika kifungo mutunza vinywaji wake mukubwa na mupishi mukubwa wa mikate, akawaweka mbele ya wakubwa wake.