Genesis 40:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yosefu akawauliza maofisa hao wa Farao waliokuwa kifungoni pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, “Mbona leo mna nyuso za huzuni?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Yusufu akawauliza maafisa hao wa Farao waliokuwa chini ya ulinzi pamoja naye nyumbani mwa bwana wake hivi, “Mbona nyuso zenu zimejaa huzuni leo?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yosefu akawauliza maofisa hao wa Farao waliokuwa kifungoni pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, “Mbona leo mna nyuso za huzuni?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yosefu akawauliza maafisa hao wa Farao waliokuwa chini ya ulinzi pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, akasema, “Mbona nyuso zenu zimejaa huzuni leo?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yusufu akawauliza maafisa hao wa Farao waliokuwa chini ya ulinzi pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, akasema, “Mbona nyuso zenu zimejaa huzuni leo?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawauliza hao maofisa wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yosefu akawauliza maofisa hao wa Farao waliokuwa kifungoni pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, “Mbona leo mna nyuso za huzuni?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawauliza hawa wafungwa wa Farao walioangaliwa naye katika nyumba ya bwana wake kwamba: Mbona leo nyuso zenu ni mbaya?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yosefu akawauliza wakubwa wale wa mufalme waliokuwa katika kifungo pamoja naye katika nyumba ya bwana wake: “Mbona leo muko na nyuso za huzuni?”