Genesis 40:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamjibu, “Tuna huzuni kwa kuwa tumeota ndoto na hakuna awezaye kututafsiria ndoto zetu.” Yosefu akawaambia, “Je, kutafsiri ndoto si kazi ya Mungu? Basi, niambieni ndoto zenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamjibu, “Sisi sote tumeota ndoto, lakini hakuna wa kuzifasiri.” Ndipo Yusufu akawaambia, “Je, kufasiri ndoto si ni kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamjibu, “Tuna huzuni kwa kuwa tumeota ndoto na hakuna awezaye kututafsiria ndoto zetu.” Yosefu akawaambia, “Je, kutafsiri ndoto si kazi ya Mungu? Basi, niambieni ndoto zenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamjibu, “Sisi sote tuliota ndoto, lakini hapakuwa na mtu ye yote wa kuzifasiri.” Ndipo Yosefu akawaambia, “Je, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamjibu, “Sisi sote tuliota ndoto, lakini hapakuwa na mtu yeyote wa kuzifasiri.” Ndipo Yusufu akawaambia, “Je, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Nawaomba mniambie, kufasiri si ni kazi ya Mungu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamjibu, “Tuna huzuni kwa kuwa tumeota ndoto na hakuna awezaye kututafsiria ndoto zetu.” Yosefu akawaambia, “Je, kutafsiri ndoto si kazi ya Mungu? Basi, niambieni ndoto zenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamwambia: Tumeota ndoto, lakini mwenye kuzifumbua hakuna. Yosefu akawaambia: Kumbe kufumbua siko kwake Mungu? Lakini nisumulieni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamujibu: “Tuna huzuni kwa sababu tumeota ndoto na hakuna anayeweza kututafsiria ndoto zetu.” Yosefu akawaambia: “Kutafsiri ndoto si kazi ya Mungu? Basi, muniambie ndoto zenu.”