Genesis 41:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati ule ulipotukasirikia sisi watumishi wako, mimi na mwoka mikate mkuu, ulitufungia ndani ya ngome ya mkuu wa kikosi cha ulinzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farao alipowakasirikia watumishi wake, alinifunga mimi na mwokaji mkuu katika nyumba ya mkuu wa walinzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Farao aliwakasirikia watumwa wake, akanitia nifungwe nyumbani mwa mkuu wa askari, mimi na mkuu wa waokaji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati ule ulipotukasirikia sisi watumishi wako, mimi na mwoka mikate mkuu, ulitufungia ndani ya ngome ya mkuu wa kikosi cha ulinzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati fulani Farao aliwakasirikia watumishi wake, akanifunga mimi na mwokaji mkuu katika nyumba ya mkuu wa ulinzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati fulani Farao aliwakasirikia watumishi wake, akanifunga mimi na mwokaji mkuu katika nyumba ya mkuu wa ulinzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Farao aliwakasirikia watumishi wake, akanitia nifungwe nyumbani mwa mkuu wa askari walinzi, mimi na mkuu wa waokaji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati ule ulipotukasirikia sisi watumishi wako, mimi na mwoka mikate mkuu, ulitufungia ndani ya ngome ya mkuu wa kikosi cha ulinzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Farao alipowakasirikia watumishi wake, alinitia katika kifungo nyumbani mwake mkuu wao wanaomlinda mfalme, mimi pamoja na mkuu wa wachoma mikate;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Farao aliwakasirikia watumwa wake, akanitia nifungwe nyumbani mwa mkuu wa askari, mimi na mkuu wa waokaji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule ulipotukasirikia sisi watumishi wako, mimi na mupishi mukubwa wa mikate, ulitufungia ndani ya nyumba ya mukubwa wa waaskari walinzi.