Genesis 41:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kijana mmoja Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa kikosi cha ulinzi, alikuwa pamoja nasi kifungoni. Tulipomsimulia ndoto zetu, yeye aliweza kututafsiria kila mmoja wetu kulingana na ndoto yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kuna kijana Mwebrania aliyekuwa pamoja nasi huko, mtumishi wa mkuu wa walinzi. Tulimweleza ndoto zetu, naye akatufasiria, akitupatia kila mtu tafsiri ya ndoto yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huko pamoja nasi palikuwa na kijana; Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kijana mmoja Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa kikosi cha ulinzi, alikuwa pamoja nasi kifungoni. Tulipomsimulia ndoto zetu, yeye aliweza kututafsiria kila mmoja wetu kulingana na ndoto yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi kijana wa Kiebrania aliyekuwa pamoja nasi huko, alikuwa mtumishi wa mkuu wa kikosi cha ulinzi. Tulimweleza ndoto zetu, naye akatufasiria, akitupa kila mtu tafsiri ya ndoto yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi kijana wa Kiebrania aliyekuwa pamoja nasi huko, alikuwa mtumishi wa mkuu wa kikosi cha ulinzi. Tulimweleza ndoto zetu, naye akatufasiria, akitupa kila mtu tafsiri ya ndoto yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huko pamoja nasi palikuwa na kijana; Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kijana mmoja Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa kikosi cha ulinzi, alikuwa pamoja nasi kifungoni. Tulipomsimulia ndoto zetu, yeye aliweza kututafsiria kila mmoja wetu kulingana na ndoto yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, mle tulikuwa na kijana wa Kiebureo, mtumwa wake mkuu wao wanaomlinda mfalme; tulipomsimulia ndoto zetu, akamfumbulia maana yao, kila mtu akamfumbuli ndoto yake yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huko pamoja nasi palikuwa na kijana; Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kijana mumoja Mwebrania, mutumishi wa jemadari wa waaskari walinzi, alikuwa pamoja nasi katika kifungo. Tulipomwelezea ndoto zetu, yeye aliweza kutuelezea kila mumoja wetu kulingana na ndoto yake.