Genesis 41:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Yosefu akamwambia Farao, “Ndoto zako zote mbili tafsiri yake ni moja. Mungu amekufunulia mambo atakayofanya hivi karibuni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Yusufu akamwambia Farao, “Ndoto za Farao ni ndoto hiyo hiyo moja. Mungu amemfunulia Farao jambo analokusudia kufanya karibuni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Yosefu akamwambia Farao, “Ndoto zako zote mbili tafsiri yake ni moja. Mungu amekufunulia mambo atakayofanya hivi karibuni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yosefu akamwambia Farao, “Ndoto za Farao ni ndoto iyo hiyo moja. Mungu amemfunulia Farao jambo analokusudia kufanya karibuni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yusufu akamwambia Farao, “Ndoto za Farao ni ndoto iyo hiyo moja. Mungu amemfunulia Farao jambo analokusudia kufanya karibuni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonesha Farao atakayoyafanya hivi karibuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Yosefu akamwambia Farao, “Ndoto zako zote mbili tafsiri yake ni moja. Mungu amekufunulia mambo atakayofanya hivi karibuni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yosefu alipomwmbia Farao: Ndoto za Farao ni moja; Mungu amemjulisha Farao atakayoyafanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yosefu akamwambia mufalme: “Ndoto zako zote mbili zina maana moja tu. Mungu amekufunulia mambo atakayofanya sasa hivi.