Genesis 41:42 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo, Farao akaivua pete yake ya mhuri kidoleni mwake na kumvisha Yosefu, akamvalisha na mavazi ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Farao akaivua pete yake ya muhuri kutoka kidoleni mwake na kuivalisha katika kidole cha Yusufu. Akamvika majoho mazuri ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo, Farao akaivua pete yake ya mhuri kidoleni mwake na kumvisha Yosefu, akamvalisha na mavazi ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Farao akaivua pete yake ya muhuri kutoka kidoleni mwake na kuivalisha katika kidole cha Yosefu. Akamvika majoho mazuri ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Farao akaivua pete yake ya muhuri kutoka kidoleni mwake na kuivalisha katika kidole cha Yusufu. Akamvika majoho mazuri ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo, Farao akaivua pete yake ya mhuri kidoleni mwake na kumvisha Yosefu, akamvalisha na mavazi ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Farao akaitoa pete yake kidoleni pake, akaitia katika kidole cha Yosefu, akamvika nguo nyeupe za bafta nzuri, akamtia mkufu wa dhahabu shingoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu, mufalme akavua pete yake ya muhuri kwenye kidole chake na kumuvalisha Yosefu. Akamuvalisha na nguo za kitani safi na mukufu wa zahabu kwa shingo.