Genesis 41:45 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Farao akampa Yosefu jina la Kimisri: Safenath-panea. Akamwoza Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni. Basi, Yosefu akaanza kuitembelea nchi nzima ya Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farao akamwita Yusufu jina Safenath-Panea; pia akampa Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni, kuwa mke wake. Ndipo Yusufu akaitembelea nchi yote ya Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe Yusufu akaenda huko na huko katika nchi yote ya Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Farao akampa Yosefu jina la Kimisri: Safenath-panea. Akamwoza Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni. Basi, Yosefu akaanza kuitembelea nchi nzima ya Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farao akamwita Yosefu Safenath-Panea, pia akampa Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni, kuwa mke wake. Ndipo Yosefu akaitembelea nchi yote ya Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farao akamwita Yusufu Safenath-Panea, pia akampa Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni, kuwa mke wake. Ndipo Yusufu akaitembelea nchi yote ya Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe. Na Yusufu akaenda huku na huko katika nchi yote ya Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Farao akampa Yosefu jina la Kimisri: Safenath-panea. Akamwoza Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni. Basi, Yosefu akaanza kuitembelea nchi nzima ya Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Farao akamwita Yosefu Safenati-Panea (Mponya Wazima), akampa Asenati, binti Potifera, mtambikaji wa Oni, kuwa mkewe. Kisha Yosefu akatoka kwenda kuzitazama nchi zote za Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe Yusufu akaenda huko na huko katika nchi yote ya Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akamupa Yosefu jina la Kimisri: Safenati-Panea. Akamupa Asenati, binti ya Potifera, kuhani wa muji wa Oni kuwa muke wake. Basi, Yosefu akaanza kutembelea inchi nzima ya Misri.