Genesis 41:46 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yosefu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kumtumikia Farao, mfalme wa Misri. Alitoka nyumbani kwa Farao na kuitembelea nchi yote ya Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yusufu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoingia katika utumishi wa Farao, mfalme wa Misri. Naye Yusufu akatoka mbele ya Farao akasafiri katika nchi yote ya Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akapita katika nchi yote ya Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yosefu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kumtumikia Farao, mfalme wa Misri. Alitoka nyumbani kwa Farao na kuitembelea nchi yote ya Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yosefu alikuwa na miaka thelathini alipoingia katika utumishi wa Farao mfalme wa Misri. Naye Yosefu akatoka mbele ya Farao akasafiri katika nchi yote ya Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yusufu alikuwa na miaka thelathini alipoingia katika utumishi wa Farao mfalme wa Misri. Naye Yusufu akatoka mbele ya Farao akasafiri katika nchi yote ya Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akasafiri katika nchi yote ya Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yosefu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kumtumikia Farao, mfalme wa Misri. Alitoka nyumbani kwa Farao na kuitembelea nchi yote ya Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, Yosefu aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri, alikuwa mwenye miaka 30, napo Yosefu alipotoka kwake Farao akatembea katika nchi zote za Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akapita katika nchi yote ya Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yosefu alikuwa na umri wa miaka makumi tatu alipoanza kumutumikia mufalme. Alitoka katika nyumba ya mufalme na kuitembelea inchi yote ya Misri.