Genesis 41:48 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yosefu akakusanya chakula chote wakati huo wa miaka saba ya shibe na kukiweka akiba katika miji ya Misri. Katika kila mji akaweka akiba ya chakula kutoka mashamba yaliyo karibu na mji huo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yusufu akakusanya chakula chote kilichozalishwa katika ile miaka saba ya shibe nchini Misri, akakihifadhi katika miji. Katika kila mji kulihifadhiwa chakula kilichozalishwa katika mashamba yaliyouzunguka mji huo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akakusanya chakula chote cha miaka ile saba katika nchi ya Misri. Akaweka chakula katika miji; chakula cha mashamba yaliyouzunguka kila mji, akakiweka ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yosefu akakusanya chakula chote wakati huo wa miaka saba ya shibe na kukiweka akiba katika miji ya Misri. Katika kila mji akaweka akiba ya chakula kutoka mashamba yaliyo karibu na mji huo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yosefu akakusanya chakula chote kilichozalishwa katika ile miaka saba ya neema nchini Misri, akakihifadhi katika ghala za miji. Katika kila mji kulihifadhiwa chakula kilichozalishwa katika mashamba yaliyouzunguka mji huo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yusufu akakusanya chakula chote kilichozalishwa katika ile miaka saba ya neema nchini Misri, akakihifadhi katika ghala za miji. Katika kila mji kulihifadhiwa chakula kilichozalishwa katika mashamba yaliyouzunguka mji huo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akakusanya chakula chote cha miaka ile saba katika nchi ya Misri. Akaweka chakula katika miji; chakula cha mashamba yaliyouzunguka kila mji, akakiweka ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yosefu akakusanya chakula chote wakati huo wa miaka saba ya shibe na kukiweka akiba katika miji ya Misri. Katika kila mji akaweka akiba ya chakula kutoka mashamba yaliyo karibu na mji huo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
naye Yosefu akavikusanya vilaji vyote vya hiyo miaka saba, iliyoipata nchi ya Misri, akavilimbika mijini akiagiza, vilaji vyote vya mashamba ya kila mji yaliyouzunguka yawekwe vyanjani mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akakusanya chakula chote cha miaka ile saba katika nchi ya Misri. Akaweka chakula katika miji; chakula cha mashamba yaliyouzunguka kila mji, akakiweka ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yosefu akakusanya chakula chote wakati ule wa miaka saba ya shibe na kukiweka akiba katika miji ya Misri. Katika kila muji akaweka akiba ya chakula kutoka mashamba yanayokuwa karibu na muji ule.