Genesis 41:55 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wananchi wa Misri walipoanza kuona njaa, walimlilia Farao awape chakula. Naye Farao akawaambia Wamisri wote, “Nendeni kwa Yosefu; atakalowaambia fanyeni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nchi yote ya Misri ilipopatwa na njaa, watu wakamlilia Farao ili awape chakula. Ndipo Farao aliwaagiza Wamisri wote, “Nendeni kwa Yusufu, nanyi mfanye anachowaambia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wananchi wa Misri walipoanza kuona njaa, walimlilia Farao awape chakula. Naye Farao akawaambia Wamisri wote, “Nendeni kwa Yosefu; atakalowaambia fanyeni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati nchi yote ya Misri ilipopatwa na njaa, watu wakamlilia Farao ili awape chakula. Ndipo Farao alipowaagiza Wamisri wote, akisema, “Nendeni kwa Yosefu, nanyi mfanye anachowaambia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati nchi yote ya Misri ilipopatwa na njaa, watu wakamlilia Farao ili awape chakula. Ndipo Farao alipowaagiza Wamisri wote, akisema, “Nendeni kwa Yusufu, nanyi mfanye anachowaambia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Nendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati wananchi wa Misri walipoanza kuona njaa, walimlilia Farao awape chakula. Naye Farao akawaambia Wamisri wote, “Nendeni kwa Yosefu; atakalowaambia fanyeni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wote wa Misri walipoona njaa wakamililia Farao, awape chakula; naye Farao akawaambia watu wote: Nendeni kwa Yosefu! Nayo atakayowaambia yafanyizeni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wanainchi wa Misri walipoanza kuona njaa, wakamulilia mufalme awape chakula. Naye akawaambia Wamisri wote: “Mwende kwa Yosefu; mufanye neno lolote atakalowaambia.”