Genesis 42:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu mdogo, wakati wengine wenu wanamngoja gerezani. Hapo ndipo maneno yenu yatakapojulikana ukweli wake. La sivyo, naapa kwa jina la Farao kwamba nyinyi ni wapelelezi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu. Wengine mtawekwa gerezani, ili maneno yenu yajaribiwe kuona kama mnasema kweli. La sivyo, hakika kama Farao aishivyo ninyi ni wapelelezi!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mpelekeni mmoja wenu, aende akamlete ndugu yenu, na ninyi mtafungwa, hata maneno yenu yahakikishwe, kama mna kweli ninyi; ikiwa sivyo, aishivyo Farao, ninyi ni wapelelezi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu mdogo, wakati wengine wenu wanamngoja gerezani. Hapo ndipo maneno yenu yatakapojulikana ukweli wake. La sivyo, naapa kwa jina la Farao kwamba nyinyi ni wapelelezi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu, wengine mtawekwa gerezani, ili maneno yenu yajaribiwe kuona kama mnasema kweli. La sivyo, hakika kama Farao aishivyo ninyi ni wapelelezi!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu, wengine mtawekwa gerezani, ili maneno yenu yajaribiwe kuona kama mnasema kweli. La sivyo, hakika kama Farao aishivyo ninyi ni wapelelezi!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtumeni mmoja wenu, aende akamlete ndugu yenu, na ninyi mtafungwa jela, hadi maneno yenu yahakikishwe kama mna kweli ninyi; ikiwa sivyo, aishivyo Farao hakika ninyi ni wapelelezi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu mdogo, wakati wengine wenu wanamngoja gerezani. Hapo ndipo maneno yenu yatakapojulikana ukweli wake. La sivyo, naapa kwa jina la Farao kwamba nyinyi ni wapelelezi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Toeni mmoja miongoni mwenu, aende kumchukua ndugu yenu! Nanyi wengine mtafungwa. Hivyo mtaumbuliwa, kama maneno yenu ni ya kweli, au kama sivyo; hivyo, Farao alivyo mzima, mu wapelelezi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mpelekeni mmoja wenu, aende akamlete ndugu yenu, na ninyi mtafungwa, hata maneno yenu yahakikishwe, kama mna kweli ninyi; ikiwa sivyo, aishivyo Farao, ninyi ni wapelelezi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutume mumoja wenu amulete yule ndugu yenu mudogo, wakati wengine wenu wanamungoja katika kifungo. Kwa hiyo ukweli wa maneno yenu utajulikana. Kama sivyo, ninaapa kwa jina la mufalme wa Misri kwamba ninyi ni wapelelezi.”