Genesis 42:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Hii hapa mdomoni mwa gunia langu!” Waliposikia hayo, wakafa moyo. Wakatazamana huku wanatetemeka na kuulizana, “Ni jambo gani hili alilotutendea Mungu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Iko ndani ya gunia langu.” Mioyo yao ikazimia, na kila mmoja akamgeukia mwenzake wakitetemeka, wakaulizana, “Ni nini hiki Mungu alichotufanyia?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia nduguze, Fedha yangu imerudishwa, angalia, imo humo guniani mwangu. Mioyo yao ikazimia, wakageukiana wakitetemeka, wakasema, N'nini hii Mungu aliyotutendea?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Hii hapa mdomoni mwa gunia langu!” Waliposikia hayo, wakafa moyo. Wakatazamana huku wanatetemeka na kuulizana, “Ni jambo gani hili alilotutendea Mungu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Iko ndani ya gunia langu.” Mioyo yao ikazimia, na kila mmoja akamgeukia mwenzake wakitetemeka, wakaulizana, “Ni nini hiki Mungu alichotufanyia?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Iko ndani ya gunia langu.” Mioyo yao ikazimia, na kila mmoja akamgeukia mwenzake wakitetemeka, wakaulizana, “Ni nini hiki Mungu alichotufanyia?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia nduguze, Fedha yangu imerudishwa, angalia, imo humo guniani mwangu. Mioyo yao ikazimia, wakageukiana wakitetemeka, wakasema, Ni nini hii Mungu aliyotutendea?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Hii hapa mdomoni mwa gunia langu!” Waliposikia hayo, wakafa moyo. Wakatazamana huku wanatetemeka na kuulizana, “Ni jambo gani hili alilotutendea Mungu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia ndugu zake: Kumbe fedha zangu zimerudishwa, zimo ndani ya gunia langu! Ndipo, mioyo yao ilipopigwa bumbuazi kwa kustuka, wakaambiana wao kwa wao: Mbona Mungu anatufanyizia haya?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia nduguze, Fedha yangu imerudishwa, angalia, imo humo guniani mwangu. Mioyo yao ikazimia, wakageukiana wakitetemeka, wakasema, N’nini hii Mungu aliyotutendea?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaambia wandugu zake: “Feza yangu imerudishwa. Ndio hii hapa kwenye kinywa cha mufuko wangu!” Waliposikia hayo, wakavunjika moyo. Wakaangalia wakiwa wanatetemeka na kuulizana: “Ni jambo gani hili Mungu alilotutendea?”