Genesis 42:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo Yosefu alikuwa ndiye mkuu huko Misri. Yeye ndiye aliyehusika na kuwauzia wananchi nafaka. Basi, kaka zake wakaja na kumwinamia Yosefu kwa heshima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo Yusufu alikuwa mtawala wa nchi ya Misri, na ndiye aliwauzia watu wote nafaka. Kwa hiyo wakati ndugu zake Yusufu walifika, wakamsujudia hadi nyuso zao zikagusa ardhi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yusufu alikuwa ni liwali juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo Yosefu alikuwa ndiye mkuu huko Misri. Yeye ndiye aliyehusika na kuwauzia wananchi nafaka. Basi, kaka zake wakaja na kumwinamia Yosefu kwa heshima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo Yosefu alikuwa mtawala wa nchi ya Misri, naye alikuwa ndiye aliyewauzia watu wote nafaka. Kwa hiyo wakati ndugu zake Yosefu walipofika, wakamsujudia hadi nyuso zao zikagusa ardhi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo Yusufu alikuwa mtawala wa nchi ya Misri, naye alikuwa ndiye aliwauzia watu wote nafaka. Kwa hiyo wakati ndugu zake Yusufu walipofika, wakamsujudia hadi nyuso zao zikagusa ardhi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yusufu alikuwa ni mkuu juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo Yosefu alikuwa ndiye mkuu huko Misri. Yeye ndiye aliyehusika na kuwauzia wananchi nafaka. Basi, kaka zake wakaja na kumwinamia Yosefu kwa heshima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Yosefu alikuwa mtawala nchi hiyo, naye ndiye aliyewauzia ngano watu wote wa nchi hiyo. Kaka zake Yosefu walipofika kwake wakamwinamia, mpaka nyuso zao zikifika chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yusufu alikuwa ni liwali juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule Yosefu alikuwa mukubwa kule Misri. Yeye ndiye aliyekuwa akiwauzishia wanainchi ngano. Basi, kaka zake wakakuja na kuinama mbele ya Yosefu kwa heshima.