Genesis 43:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Israeli, baba yao, akawaambia, “Haya! Kwa vile ni lazima iwe hivyo basi, fanyeni hivi: Chukueni katika mifuko yenu baadhi ya mazao bora ya nchi yetu, mkampelekee zawadi huyo mkuu. Mchukulieni mafuta kidogo ya mkwaju, asali kidogo, ubani, manemane, kungu na lozi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi baba yao Israeli akawaambia, “Kama ni lazima iwe hivyo, basi fanyeni hivi: Wekeni sehemu ya bidhaa bora za nchi katika mifuko yenu, na mmpelekee yule mtu kama zawadi: zeri kidogo, asali kidogo, vikolezo, manemane, kungu na lozi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Israeli, baba yao, akawaambia, “Haya! Kwa vile ni lazima iwe hivyo basi, fanyeni hivi: chukueni katika mifuko yenu baadhi ya mazao bora ya nchi yetu, mkampelekee zawadi huyo mkuu. Mchukulieni mafuta kidogo ya mkwaju, asali kidogo, ubani, manemane, kungu na lozi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi baba yao Israeli akawaambia, “Kama ni lazima iwe hivyo, basi fanyeni hivi: Wekeni baadhi ya mazao bora ya nchi katika mifuko yenu na mpelekeeni yule mtu kama zawadi, zeri kidogo, asali kidogo, vikolezo, manemane, kungu na lozi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi baba yao Israeli akawaambia, “Kama ni lazima iwe hivyo, basi fanyeni hivi: Wekeni baadhi ya mazao bora ya nchi katika mifuko yenu na mpelekeeni yule mtu kama zawadi, zeri kidogo, asali kidogo, vikolezo, manemane, kungu na lozi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Israeli, baba yao, akawaambia, “Haya! Kwa vile ni lazima iwe hivyo basi, fanyeni hivi: Chukueni katika mifuko yenu baadhi ya mazao bora ya nchi yetu, mkampelekee zawadi huyo mkuu. Mchukulieni mafuta kidogo ya mkwaju, asali kidogo, ubani, manemane, kungu na lozi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, baba yao Isiraeli akawaitikia kwamba: Kama hayana budi kuwa hivyo, haya! Yafanyizeni! Chukueni vyomboni mwenu mazao ya nchi hii yanayosifiwa, tena mpelekeeni yule mtu kuwa matunzo yake: mafuta ya mkwaju machache na asali kidogo na manukato na uvumba na kungu na lozi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo Israeli, baba yao, akawaambia: “Basi! Kwa vile ni lazima ikuwe hivyo basi, mufanye hivi: mutwae katika mifuko yenu sehemu ya mazao bora ya inchi yetu, mumupelekee zawadi yule mukubwa. Mumupelekee mafuta kidogo ya mukwaju, asali kidogo, ubani, marasi, kungu na lozi.