Genesis 43:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, wakachukua zile zawadi, na fedha mara mbili ya zile za awali, wakaenda Misri pamoja na ndugu yao Benyamini. Walipowasili, wakaenda na kusimama mbele ya Yosefu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi hao watu wakazichukua zile zawadi na zile fedha mara mbili pamoja na Benyamini. Wakafanya haraka kwenda Misri na wakajionesha kwa Yusufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hao watu wakatwaa zawadi ile, wakatwaa na fedha maradufu mikononi mwao, na Benyamini; wakaondoka, wakashuka mpaka Misri, wakasimama mbele ya Yusufu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, wakachukua zile zawadi, na fedha mara mbili ya zile za awali, wakaenda Misri pamoja na ndugu yao Benyamini. Walipowasili, wakaenda na kusimama mbele ya Yosefu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi hao watu wakazichukua zile zawadi na zile fedha mara mbili pamoja na Benyamini. Wakafanya haraka kwenda Misri na walipofika wakajionyesha kwa Yosefu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi hao watu wakazichukua zile zawadi na zile fedha mara mbili pamoja na Benyamini. Wakafanya haraka kwenda Misri na walipofika wakajionyesha kwa Yusufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hao watu wakatwaa zawadi ile, wakatwaa na fedha maradufu mikononi mwao, na Benyamini; wakaondoka, wakashuka mpaka Misri, wakasimama mbele ya Yusufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, wakachukua zile zawadi, na fedha mara mbili ya zile za awali, wakaenda Misri pamoja na ndugu yao Benyamini. Walipowasili, wakaenda na kusimama mbele ya Yosefu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha hao watu wakayachukua hayo matunzo, nazo fedha za mara mbili wakazichukua mikononi mwao, naye Benyamini, wakaondoka kutelemka kwenda Misri. Walipomtokea Yosefu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hao watu wakatwaa zawadi ile, wakatwaa na fedha maradufu mikononi mwao, na Benyamini; wakaondoka, wakashuka mpaka Misri, wakasimama mbele ya Yusufu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wakatwaa zile zawadi na feza mara mbili ya ile ya mbele, wakakwenda Misri pamoja na ndugu yao Benjamina. Walipofika, wakakwenda na kusimama mbele ya Yosefu.