Genesis 43:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipoona wamepelekwa nyumbani kwa Yosefu, wakashikwa na hofu, wakasema wao kwa wao, “Tumeletwa huku kwa sababu ya ile fedha tuliyorudishiwa katika magunia yetu tulipokuja safari ya kwanza ili apate kisingizio cha kutushambulia ghafla na kutunyanganya punda wetu na kutufanya watumwa wake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi watu hao wakaogopa walipopelekwa nyumbani mwa Yusufu. Wakafikiri, “Tumeletwa hapa kwa ajili ya zile fedha zilizorudishwa katika magunia yetu mara ile ya kwanza. Anataka kutushambulia na kutushinda, atuchukue sisi kama watumwa, na atwae hawa punda wetu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini watu hao wakaogopa kwa sababu wameletwa nyumbani mwa Yusufu, wakasema, Kwa sababu ya fedha zile zilizorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tumeletwa humu; apate kutushitaki, na kutuangukia, atutwae sisi kuwa watumwa, na punda zetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipoona wamepelekwa nyumbani kwa Yosefu, wakashikwa na hofu, wakasema wao kwa wao, “Tumeletwa huku kwa sababu ya ile fedha tuliyorudishiwa katika magunia yetu tulipokuja safari ya kwanza ili apate kisingizio cha kutushambulia ghafla na kutunyang'anya punda wetu na kutufanya watumwa wake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi watu hao wakaogopa walipopelekwa nyumbani kwa Yosefu. Wakafikiri, “Tumeletwa hapa kwa ajili ya zile fedha zilizorudishwa katika magunia yetu mara ile ya kwanza. Anataka kutushambulia na kutushinda, atuchukue sisi kama watumwa, na atwae hawa punda zetu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi watu hao wakaogopa walipopelekwa nyumbani kwa Yusufu. Wakafikiri, “Tumeletwa hapa kwa ajili ya zile fedha zilizorudishwa katika magunia yetu mara ile ya kwanza. Anataka kutushambulia na kutushinda, atuchukue sisi kama watumwa, na atwae hawa punda zetu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini watu hao wakaogopa kwa sababu wameletwa nyumbani mwa Yusufu, wakasema, Kwa sababu ya fedha zile zilizorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tumeletwa humu; apate kutushitaki, na kutushika, atutwae sisi kuwa watumwa, na punda wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipoona wamepelekwa nyumbani kwa Yosefu, wakashikwa na hofu, wakasema wao kwa wao, “Tumeletwa huku kwa sababu ya ile fedha tuliyorudishiwa katika magunia yetu tulipokuja safari ya kwanza ili apate kisingizio cha kutushambulia ghafla na kutunyanganya punda wetu na kutufanya watumwa wake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watu hao wakashikwa na woga kwa kuingizwa nyumbani mwake Yosefu, wakasema: Tumeingizwa humu kwa ajili ya hizo fedha zilizorudishwa hapo kwanza katika magunia yetu, apate kutusingizia na kutulipisha yaliyotuangukia, atuchukue sisi pamoja na punda wetu, tuwe watumwa wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini watu hao wakaogopa kwa sababu wameletwa nyumbani mwa Yusufu, wakasema, Kwa sababu ya fedha zile zilizorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tumeletwa humu; apate kutushitaki, na kutuangukia, atutwae sisi kuwa watumwa, na punda zetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipoona wamepelekwa kwenye nyumba ya Yosefu, wakashikwa na hofu, wakasema wao kwa wao: “Tumeletwa huku kwa sababu ya ile feza tuliyorudishiwa katika mifuko yetu tulipokuja safari ya kwanza kusudi apate kisingizio cha kutushambulia kwa rafla na kutunyanganya punda wetu na kutufanya watumwa wake.”