Genesis 43:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tulipofika mahali pa kulala wageni huko njiani, tulifungua magunia yetu, tukashangaa kukuta fedha ya kila mmoja wetu mdomoni mwa gunia lake bila kuguswa. Sasa tumeirudisha fedha hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mahali pale tulipotua wakati wa jioni tulifungua magunia yetu, na kila mmoja wetu akakuta fedha zake katika gunia lake, kiasi kile kile tulicholeta. Kwa hiyo tumezirudisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, tulipofika nyumba ya wageni, tukafungua magunia yetu, kumbe! Fedha za kila mtu zilikuwako kinywani mwa gunia lake, fedha zetu kwa uzani wake kamili; nasi tumezileta tena mikononi mwetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tulipofika mahali pa kulala wageni huko njiani, tulifungua magunia yetu, tukashangaa kukuta fedha ya kila mmoja wetu mdomoni mwa gunia lake bila kuguswa. Sasa tumeirudisha fedha hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mahali pale tulipotua wakati wa jioni tulifungua magunia yetu, na kila mmoja wetu akakuta fedha zake, kwenye mdomo wa gunia lake kiasi kile kile tulicholeta. Kwa hiyo tumezirudisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mahali pale tulipotua wakati wa jioni tulifungua magunia yetu, na kila mmoja wetu akakuta fedha zake, kwenye mdomo wa gunia lake kiasi kile kile tulicholeta. Kwa hiyo tumezirudisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, tulipofika nyumba ya wageni, tukafungua magunia yetu, kumbe! Fedha za kila mtu zilikuwako kinywani mwa gunia lake, fedha zetu kwa uzani wake kamili; nasi tumezileta tena mikononi mwetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tulipofika mahali pa kulala wageni huko njiani, tulifungua magunia yetu, tukashangaa kukuta fedha ya kila mmoja wetu mdomoni mwa gunia lake bila kuguswa. Sasa tumeirudisha fedha hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nasi tulipofika kambini, tukafungua magunia yetu, tukaona kila mtu fedha zake juu ndani ya gunia lake, nazo hizo fedha zetu zilikuwa zenye kipimo chao sawasawa, kwa hiyo tumezirudisha mikononi mwetu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, tulipofika nyumba ya wageni, tukafungua magunia yetu, kumbe! Fedha za kila mtu zilikuwako kinywani mwa gunia lake, fedha zetu kwa uzani wake kamili; nasi tumezileta tena mikononi mwetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tulipofika pahali pa kulala wageni kule katika njia, tukafungua mifuko yetu, tukashangaa kukuta feza ya kila mumoja wetu kwenye kinywa cha mufuko wake bila kuguswa. Sasa tumerudisha feza hiyo.