Genesis 43:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule msimamizi akawajibu, “Msiwe na wasiwasi, wala msiogope. Bila shaka Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, ndiye aliyewarudishieni fedha katika magunia yenu. Mimi nilipokea fedha yenu.” Kisha akawaletea Simeoni, ndugu yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaambia, “Vema, msiogope. Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, amewapa ninyi hazina katika magunia yenu; mimi nilipokea fedha yenu.” Ndipo akawaletea Simeoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope; Mungu wenu, naye ni Mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu; fedha zenu ziliniwasilia. Kisha akawatolea Simeoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule msimamizi akawajibu, “Msiwe na wasiwasi, wala msiogope. Bila shaka Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, ndiye aliyewarudishieni fedha katika magunia yenu. Mimi nilipokea fedha yenu.” Kisha akawaletea Simeoni, ndugu yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaambia, “Vema msiogope. Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, amewapa ninyi hazina katika magunia yenu; mimi nilipokea fedha yenu.” Ndipo akawaletea Simeoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaambia, “Vema, msiogope. Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, amewapa ninyi hazina katika magunia yenu; mimi nilipokea fedha yenu.” Ndipo akawaletea Simeoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope; Mungu wenu, naye ni Mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu; fedha zenu zilinifikia. Kisha akawatolea Simeoni kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule msimamizi akawajibu, “Msiwe na wasiwasi, wala msiogope. Bila shaka Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, ndiye aliyewarudishieni fedha katika magunia yenu. Mimi nilipokea fedha yenu.” Kisha akawaletea Simeoni, ndugu yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akasema: Tulieni tu, msiogope! Mungu wenu na Mungu wa baba yenu aliwapatia kilimbiko katika magunia yenu, fedha zenu zilifika kwangu. Kisha akamfungua Simeoni, akamleta kwao,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope; Mungu wenu, naye ni Mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu; fedha zenu ziliniwasilia. Kisha akawatolea Simeoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule musimamizi akawajibu: “Musikuwe na wasiwasi, wala musiogope. Bila shaka Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, ndiye aliyewarudishia feza katika mifuko yenu. Mimi nilipokea feza yenu.” Kisha akawaletea Simeoni, ndugu yao.