Genesis 43:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ghafla, Yosefu akatoka mahali hapo, kwani machozi yalikuwa yanamlengalenga kwa shauku kubwa juu ya ndugu yake, akaingia chumbani mwake na kuangua kilio.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akiwa ameguswa sana kwa kumwona ndugu yake, Yusufu akaondoka kwa haraka na kutafuta mahali pa kulilia. Akaingia kwenye chumba chake cha pekee na kulilia humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yusufu akafanya haraka, kwa sababu moyo wake ulimwonea shauku nduguye, akatafuta pa kulia, akaingia chumbani mwake, akalia humo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ghafla, Yosefu akatoka mahali hapo, kwani machozi yalikuwa yanamlengalenga kwa shauku kubwa juu ya ndugu yake, akaingia chumbani mwake na kuangua kilio.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akiwa ameguswa sana kwa kumwona ndugu yake, Yosefu akatoka nje kwa haraka na kutafuta mahali pa kulilia. Akaingia kwenye chumba chake cha pekee na kulilia humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akiwa ameguswa sana kwa kumwona ndugu yake, Yusufu akatoka nje kwa haraka na kutafuta mahali pa kulilia. Akaingia kwenye chumba chake cha pekee na kulilia humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yusufu akafanya haraka, kwa sababu moyo wake ulimwonea shauku nduguye, akatafuta pa kulilia, akaingia chumbani mwake, akalilia humo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ghafla, Yosefu akatoka mahali hapo, kwani machozi yalikuwa yanamlengalenga kwa shauku kubwa juu ya ndugu yake, akaingia chumbani mwake na kuangua kilio.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yosefu akakimbilia chumba kingine, apate kulia machozi, kwani alichafukwa na moyo kwa kumfurahia nduguye, namo mle chumbani machozi yakamtoka kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yusufu akafanya haraka, kwa sababu moyo wake ulimwonea shauku nduguye, akatafuta pa kulia, akaingia chumbani mwake, akalia humo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yosefu akatoka pahali pale kwa haraka, kwa sababu ya hamu kubwa juu ya ndugu yake, akatafuta pahali pa kulilia. Akaingia ndani ya chumba chake na kuanza kulia.