Genesis 43:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu zake Yosefu waliketi mbele yake kulingana na umri wao, kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho, wakawa wanaangaliana kwa mshangao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu hao walikuwa wameketi mbele yake kwa mfuatano wa umri wao, kuanzia mzaliwa wa kwanza hadi mzaliwa wa mwisho, wakatazamana wao kwa wao kwa mshangao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaketi mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa cheo cha kuzaliwa kwake, na mdogo kwa udogo wake; watu hao wakastaajabu wao kwa wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu zake Yosefu waliketi mbele yake kulingana na umri wao, kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho, wakawa wanaangaliana kwa mshangao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu hao walikuwa wameketi mbele yake kwa mfuatano wa umri wao, kuanzia mzaliwa wa kwanza hadi mzaliwa wa mwisho, wakatazamana wao kwa wao kwa mshangao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu hao walikuwa wameketi mbele yake kwa mfuatano wa umri wao, kuanzia mzaliwa wa kwanza hadi mzaliwa wa mwisho, wakatazamana wao kwa wao kwa mshangao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaketi mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa haki ya uzawa wake, na mdogo kwa udogo wake; watu hao wakastaajabu wao kwa wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu zake Yosefu waliketi mbele yake kulingana na umri wao, kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho, wakawa wanaangaliana kwa mshangao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakawakalisha mbele yake, kama walivyofuatana: aliyezaliwa wa kwanza hapo palipoupasa ukubwa wake, naye mdogo hapo palipoupasa ujana wake; kwa hiyo hao watu wakastaajabu na kutazamana wao kwa wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaketi mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa cheo cha kuzaliwa kwake, na mdogo kwa udogo wake; watu hao wakastaajabu wao kwa wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu za Yosefu waliikaa mbele yake kulingana na umri wao, kuanzia wa kwanza mpaka wa mwisho. Wakakuwa wanaangaliana kwa mushangao.