Genesis 43:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Chakula kilikuwa kikichukuliwa kutoka mezani pa Yosefu na kupelekwa kwao, lakini Benyamini alipewa mara tano zaidi ya kiasi walichopewa ndugu zake. Basi, wakanywa na kufurahi pamoja naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipopelekewa sehemu ya chakula kutoka meza ya Yusufu, sehemu ya Benyamini ilikuwa mara tano zaidi ya sehemu ya wale wengine. Kwa hiyo wakanywa na kufurahi pamoja naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara tano kuliko zao. Wakanywa, wakafanya furaha pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Chakula kilikuwa kikichukuliwa kutoka mezani pa Yosefu na kupelekwa kwao, lakini Benyamini alipewa mara tano zaidi ya kiasi walichopewa ndugu zake. Basi, wakanywa na kufurahi pamoja naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati walipopelekewa sehemu ya chakula kutoka mezani mwa Yosefu, sehemu ya Benyamini ilikuwa mara tano zaidi ya sehemu ya wale wengine. Kwa hiyo wakanywa na kufurahi pamoja naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati walipelekewa sehemu ya chakula kutoka mezani mwa Yusufu, sehemu ya Benyamini ilikuwa mara tano zaidi ya sehemu ya wale wengine. Kwa hiyo wakanywa na kufurahi pamoja naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara tano kuliko zao. Wakanywa, wakafurahi pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Chakula kilikuwa kikichukuliwa kutoka mezani pa Yosefu na kupelekwa kwao, lakini Benyamini alipewa mara tano zaidi ya kiasi walichopewa ndugu zake. Basi, wakanywa na kufurahi pamoja naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakawapa vyakula vilivyotoka mezani pake Yosefu, lakini Benyamini akaandaliwa vyakula vilivyovipita vyao wote kwa wingi mara tano. Kisha wakanywa, hata wakachangamshwa pamoja naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara tano kuliko zao. Wakanywa, wakafanya furaha pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Chakula kilikuwa kikitwaliwa kutoka kwenye meza ya Yosefu na kupelekwa kwao, lakini Benjamina alipewa mara tano zaidi ya kipimo wandugu zake walichopewa. Basi, wakakunywa na kufurahi pamoja naye.