Genesis 43:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yuda akamwambia Israeli, baba yake, “Niruhusu mimi niende naye ili tuondoke mara moja, tuende tukanunue chakula, tusije tukafa njaa pamoja nawe na watoto wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Yuda akamwambia baba yake Israeli, “Mtume kijana pamoja nami, nasi tutaondoka mara moja, ili sisi na wewe pamoja na watoto wetu tuweze kuishi, wala tusife.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yuda akamwambia Israeli babaye, Mpeleke kijana pamoja nami, tuondoke, tuende zetu, ili tupate kuishi, wala tusife, sisi na wewe na watoto wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yuda akamwambia Israeli, baba yake, “Niruhusu mimi niende naye ili tuondoke mara moja, tuende tukanunue chakula, tusije tukafa njaa pamoja nawe na watoto wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yuda akamwambia baba yake Israeli, “Mtume kijana pamoja nami, nasi tutaondoka mara, ili sisi na wewe pamoja na watoto wetu tuweze kuishi, wala tusife.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yuda akamwambia baba yake Israeli, “Mtume kijana pamoja nami, nasi tutaondoka mara, ili sisi na wewe pamoja na watoto wetu tuweze kuishi, wala tusife.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yuda akamwambia Israeli baba yake, Mtume kijana pamoja nami, tuondoke, tuende zetu, ili tupate kuishi, wala tusife, sisi na wewe na watoto wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yuda akamwambia Israeli, baba yake, “Niruhusu mimi niende naye ili tuondoke mara moja, tuende tukanunue chakula, tusije tukafa njaa pamoja nawe na watoto wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Yuda akamwambia baba yake Isiraeli: Mtume huyu kijana kwenda na mimi, tupate kuondoka kwenda huko, tupone, tusife sisi na wewe na watoto wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yuda akamwambia Israeli babaye, Mpeleke kijana pamoja nami, tuondoke, tuende zetu, ili tupate kuishi, wala tusife, sisi na wewe na watoto wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yuda akamwambia baba yake Israeli: “Uniruhusu mimi niende naye kusudi tuondoke mara moja, tuende tununue chakula, tusikufe na njaa pamoja nawe na watoto wetu.