Genesis 43:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi mwenyewe nitakuwa mdhamini wake. Wewe utanidai mimi. Nisipomrudisha ukamwona kwa macho yako mwenyewe, lawama na iwe juu yangu milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi mwenyewe nitakuhakikishia usalama wake; mimi mwenyewe nitawajibika kumrudisha. Nisipomrudisha kwako na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye lawama mbele yako maisha yangu yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi nitakuwa mdhamini wake, umtake mkononi mwangu. Nisipomleta tena kwako, na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye hatia mbele yako daima;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi mwenyewe nitakuwa mdhamini wake. Wewe utanidai mimi. Nisipomrudisha ukamwona kwa macho yako mwenyewe, lawama na iwe juu yangu milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi mwenyewe nitakuhakikishia usalama wake, mimi mwenyewe nitawajibika kumrudisha. Ikiwa sitamrudisha kwako na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye lawama mbele yako maisha yangu yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi mwenyewe nitakuhakikishia usalama wake, mimi mwenyewe nitawajibika kumrudisha. Ikiwa sitamrudisha kwako na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye lawama mbele yako maisha yangu yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi nitakuwa mdhamini wake, umtake mkononi mwangu. Nisipomleta tena kwako, na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye hatia mbele yako daima;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi mwenyewe nitakuwa mdhamini wake. Wewe utanidai mimi. Nisipomrudisha ukamwona kwa macho yako mwenyewe, lawama na iwe juu yangu milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi na niwe mdhamini wake, na umtafute mkononi mwangu! Nisipomrudisha na kumsimamisha mbele yako nitakuwa nimekukosea siku zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi nitakuwa mdhamini wake, umtake mkononi mwangu. Nisipomleta tena kwako, na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye hatia mbele yako daima;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi mwenyewe nitakuwa rehani kwake. Wewe utanidai mimi. Nisipomurudisha umwone kwa macho yako mwenyewe, kosa likuwe juu yangu milele.