Genesis 44:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yuda akamjibu, “Tukuambie nini bwana? Tuseme nini kuonesha kwamba hatuna hatia? Mungu ameyafichua makosa yetu, sisi watumishi wako. Sasa sote tu watumwa wako, sisi pamoja na yule aliyepatikana na kikombe chako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yuda akajibu, “Tuseme nini kwa bwana wangu? Tutaweza kuzungumza nini? Tutawezaje kuthibitisha kwamba hatuna hatia? Mungu amefunua hatia ya watumishi wako. Sasa sisi tu watumwa wa bwana wangu, sisi pamoja na yule aliyepatikana na kikombe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yuda akasema, Tumwambie nini bwana wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yuda akamjibu, “Tukuambie nini bwana? Tuseme nini kuonesha kwamba hatuna hatia? Mungu ameyafichua makosa yetu, sisi watumishi wako. Sasa sote tu watumwa wako, sisi pamoja na yule aliyepatikana na kikombe chako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yuda akajibu, “Tutaweza kusema nini kwa bwana wangu? Tutaweza kuzungumza nini? Tutawezaje kuthibitisha kwamba hatuna hatia? Mungu amefunua hatia ya watumishi wako. Sasa sisi tu watumwa wa bwana wangu, sisi wenyewe pamoja na yule aliyepatikana na kikombe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yuda akajibu, “Tutaweza kusema nini kwa bwana wangu? Tutaweza kuzungumza nini? Tutawezaje kuthibitisha kwamba hatuna hatia? Mungu amefunua hatia ya watumishi wako. Sasa sisi tu watumwa wa bwana wangu, sisi wenyewe pamoja na yule aliyepatikana na kikombe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yuda akasema, Tumwambie nini bwana wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yuda akamjibu, “Tukuambie nini bwana? Tuseme nini kuonesha kwamba hatuna hatia? Mungu ameyafichua makosa yetu, sisi watumishi wako. Sasa sote tu watumwa wako, sisi pamoja na yule aliyepatikana na kikombe chako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yuda akajibu: Tumwambie nini bwana wetu? Tusemeje? Tutawezaje kujikania? Mngu anayaumbua maovu, watumwa wako waliyoyafanya; tazama, sisi pamoja naye aliyeonekana kuwa nacho hicho kikombe mkononi mwake tu watumwa wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yuda akasema, Tumwambie nini bwana wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yuda akamujibu: “Tukuambie nini bwana? Tuseme nini kwa kuonyesha kwamba hatuna kosa? Mungu ameyafichua makosa yetu, sisi watumishi wako. Sasa sisi wote tuko watumwa wako, sisi pamoja na yule aliyepatikana na kikombe chako.”