Genesis 44:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokuwa wamesafiri mwendo mfupi tu kutoka mjini, Yosefu alimwambia msimamizi wa nyumba yake, “Haraka! Wafuate wale watu, na utakapowakuta, uwaulize, ‘Kwa nini mmelipa mema mliyotendewa kwa maovu? Kwa nini mmeiba kikombe cha bwana wangu ambacho
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kabla hawajafika mbali kutoka mjini, Yusufu akamwambia mtumishi wake, “Wafuatilie wale watu mara moja; utakapowakuta, waambie, ‘Kwa nini mmelipiza wema kwa ubaya?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na walipotoka mjini, wala hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokuwa wamesafiri mwendo mfupi tu kutoka mjini, Yosefu alimwambia msimamizi wa nyumba yake, “Haraka! Wafuate wale watu, na utakapowakuta, uwaulize, ‘Kwa nini mmelipa mema mliyotendewa kwa maovu? Kwa nini mmeiba kikombe cha bwana wangu ambacho
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kabla hawajafika mbali kutoka mjini, Yosefu akamwambia mtumishi wake, “Wafuatilie wale watu mara moja, utakapowakuta, waambie, ‘Kwa nini mmelipiza wema kwa ubaya?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kabla hawajafika mbali kutoka mjini, Yusufu akamwambia mtumishi wake, “Wafuatilie wale watu mara moja, utakapowakuta, waambie, ‘Kwa nini mmelipiza wema kwa ubaya?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na walipotoka mjini, kabla hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokuwa wamesafiri mwendo mfupi tu kutoka mjini, Yosefu alimwambia msimamizi wa nyumba yake, “Haraka! Wafuate wale watu, na utakapowakuta, uwaulize, ‘Kwa nini mmelipa mema mliyotendewa kwa maovu? Kwa nini mmeiba kikombe cha bwana wangu ambacho
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwisha kutoka mjini na kwenda mbali kidogo, ndipo, Yosefu alipomwambia mkuu wa nyumba yake: Ondoka, uwafuate hao watu na kupiga mbio! Utakapowapata waambie: Mbona hayo mema mliyofanyiziwa mnayalipa na kufanya mabaya?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na walipotoka mjini, wala hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokuwa wamesafiri mwendo mufupi tu kutoka muji, Yosefu akamwambia musimamizi wa nyumba yake: “Haraka! Ufuate wale watu, na utakapowakuta, uwaulize: ‘Kwa nini mumelipa mema muliyotendewa kwa maovu? Kwa nini mumeiba kikombe cha bwana wangu ambacho