Genesis 44:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kumbuka, bwana, fedha tuliyokuta katika midomo ya magunia yetu tuliirudisha kutoka katika nchi ya Kanaani. Itawezekanaje tena tuibe fedha au dhahabu nyumbani mwa bwana wako?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama, tulikurudishia zile fedha kutoka nchi ya Kanaani ambazo tulizikuta kwenye magunia yetu. Hivyo, kwa nini tuibe fedha au dhahabu kutoka nyumbani mwa bwana wako?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hasha! Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu, tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa bwana wako fedha au dhahabu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kumbuka, bwana, fedha tuliyokuta katika midomo ya magunia yetu tuliirudisha kutoka katika nchi ya Kanaani. Itawezekanaje tena tuibe fedha au dhahabu nyumbani mwa bwana wako?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo tulikurudishia zile fedha kutoka nchi ya Kanaani ambazo tulizikuta kwenye midomo ya magunia yetu. Hivyo kwa nini tuibe fedha au dhahabu kutoka nyumbani kwa bwana wako?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo tulikurudishia zile fedha kutoka nchi ya Kanaani ambazo tulizikuta kwenye midomo ya magunia yetu. Hivyo kwa nini tuibe fedha au dhahabu kutoka nyumbani kwa bwana wako?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa Bwana wako fedha au dhahabu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kumbuka, bwana, fedha tuliyokuta katika midomo ya magunia yetu tuliirudisha kutoka katika nchi ya Kanaani. Itawezekanaje tena tuibe fedha au dhahabu nyumbani mwa bwana wako?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama! Hizo fedha, tulizoziona juu ndani ya magunia, tumezirudisha kwako toka nchi ya Kanaani. Tutawezaje kuiba fedha au dhahabu nyumbani mwa bwana wako?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hasha! Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu, tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa bwana wako fedha au dhahabu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kumbuka, bwana, feza tuliyokuta katika kinywa cha mifuko yetu tuliirudisha kutoka katika inchi ya Kanana. Itawezekana namna gani tena tuibe feza au zahabu kutoka nyumba ya bwana wako?