Genesis 45:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliwapa kila mmoja wao mavazi ya kubadili, lakini akampa Benyamini vipande 300 vya fedha na mavazi matano ya kubadili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akampa kila mmoja mavazi mapya, lakini Benyamini akampa shekeli mia tatu za fedha, na jozi tano za nguo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawapa kila mtu nguo za kubadili; lakini Benyamini, alimpa fedha mia tatu na mavazi matano ya kubadili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliwapa kila mmoja wao mavazi ya kubadili, lakini akampa Benyamini vipande 300 vya fedha na mavazi matano ya kubadili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mmoja mavazi mapya, lakini Benyamini akampa shekeli 300 za fedha, na jozi tano za nguo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mmoja mavazi mapya, lakini Benyamini akampa shekeli 300 za fedha, na jozi tano za nguo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawapa kila mtu nguo za kubadili; lakini Benyamini, alimpa fedha mia tatu na mavazi matano ya kubadili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliwapa kila mmoja wao mavazi ya kubadili, lakini akampa Benyamini vipande 300 vya fedha na mavazi matano ya kubadili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wote akawapa nguo za zikukuu, kila mmoja yake; lakini Benyamini akampa fedha 300 na nguo tano za sikukuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawapa kila mtu nguo za kubadili; lakini Benyamini, alimpa fedha mia tatu na mavazi matano ya kubadili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliwapa kila mumoja wao nguo za kubadilisha, lakini akamupa Benjamina vikoroti mia tatu vya feza na nguo tano za kubadilisha.