Genesis 45:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, walipomsimulia yote waliyoagizwa na Yosefu na alipoyaona magari aliyopelekewa na Yosefu kumchukua, moyo wake ukajaa furaha kupita kiasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini walipokwisha kumweleza kila kitu ambacho Yusufu alikuwa amewaambia, na alipoona magari ya kukokotwa Yusufu aliyokuwa amempelekea ya kumchukua aende Misri, roho ya baba yao Yakobo ikahuishwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyoyapeleka Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, walipomsimulia yote waliyoagizwa na Yosefu na alipoyaona magari aliyopelekewa na Yosefu kumchukua, moyo wake ukajaa furaha kupita kiasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini walipokwisha kumweleza kila kitu ambacho Yosefu alikuwa amewaambia, na alipoona magari ya kukokotwa Yosefu aliyokuwa amempelekea ya kumchukua aende Misri, roho ya baba yao Yakobo ikahuishwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini walipokwisha kumweleza kila kitu ambacho Yusufu alikuwa amewaambia, na alipoona magari ya kukokotwa Yusufu aliyokuwa amempelekea ya kumchukua aende Misri, roho ya baba yao Yakobo ikahuishwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyotuma Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, walipomsimulia yote waliyoagizwa na Yosefu na alipoyaona magari aliyopelekewa na Yosefu kumchukua, moyo wake ukajaa furaha kupita kiasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamwambia maneno yote, Yosefu aliyowaambia; naye alipoyaona hayo magari, Yosefu aliyoyatuma kumchukua, ndipo, roho yake ilipomrudia baba yao Yakobo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyoyapeleka Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, walipomwelezea yote waliagizwa na Yosefu na alipoona magari aliyopelekewa na Yosefu kwa kumubeba, moyo wake ukajaa furaha kupita kiasi.