Genesis 45:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yosefu. Je, baba yangu angali hai?” Lakini ndugu zake wakapigwa na bumbuazi mbele yake, hata wakashindwa kumjibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yusufu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yusufu! Je, baba yangu angali hai bado?” Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yosefu. Je, baba yangu angali hai?” Lakini ndugu zake wakapigwa na bumbuazi mbele yake, hata wakashindwa kumjibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yosefu! Je, baba yangu angali hai bado?” Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yusufu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yusufu! Je, baba yangu angali hai bado?” Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yosefu. Je, baba yangu angali hai?” Lakini ndugu zake wakapigwa na bumbuazi mbele yake, hata wakashindwa kumjibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yosefu akawaambia ndugu zake: Ni mimi Yosefu! Baba yangu yuko mzima bado? Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwani walimstukia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yosefu akawaambia wandugu zake: “Mimi ni Yosefu. Baba yangu angali muzima?” Lakini wandugu zake wakapigwa na bumbuazi mbele yake, hata wakashindwa kumujibu.