Genesis 46:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yosefu akapanda gari lake la farasi, akaenda kumlaki Israeli, baba yake, huko Gosheni. Alipomfikia baba yake, alimkumbatia na kulia kwa kitambo kirefu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yusufu aliandaa gari lake la vita, na akaenda Gosheni kumlaki baba yake, Israeli. Mara Yusufu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionyesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kizima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yosefu akapanda gari lake la farasi, akaenda kumlaki Israeli, baba yake, huko Gosheni. Alipomfikia baba yake, alimkumbatia na kulia kwa kitambo kirefu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
gari kubwa zuri la Yosefu liliandaliwa, naye akaenda Gosheni kumlaki baba yake Israeli. Mara Yosefu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
gari kubwa zuri la Yusufu liliandaliwa, naye akaenda Gosheni kumlaki baba yake Israeli. Mara Yusufu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kirefu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yosefu akapanda gari lake la farasi, akaenda kumlaki Israeli, baba yake, huko Gosheni. Alipomfikia baba yake, alimkumbatia na kulia kwa kitambo kirefu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yosefu alipolitandika gari lake, akamwendea baba yake Isiraeli huko Goseni. Alipomwonekea, akamkumbatia shingoni akalia machozi hapo shingoni pake kitambo kizima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionyesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kizima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yosefu akapanda gari lake la farasi, akakwenda kumupokea baba yake Israeli, kule Goseni. Alipomufikia baba yake, alimukumbatia na kulia kwa kitambo kirefu.