Genesis 46:32 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitamweleza kwamba nyinyi ni wachungaji kwani mmekuwa mkichunga mifugo, na kwamba mmewasili pamoja na mbuzi, kondoo, ng'ombe na mali yenu yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu hao ni wafugaji; wao huchunga mifugo, na wamekuja na makundi ya kondoo, mbuzi na ng’ombe, pamoja na kila kitu walicho nacho.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watu hao ni wachungaji, maana wamekuwa watu wa kuchunga wanyama, nao wameleta kondoo zao, na ng'ombe zao, na yote waliyo nayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitamweleza kwamba nyinyi ni wachungaji kwani mmekuwa mkichunga mifugo, na kwamba mmewasili pamoja na mbuzi, kondoo, ng'ombe na mali yenu yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu hao ni wachunga mifugo, huchunga mifugo, wamekuja na makundi ya kondoo, mbuzi na ng'ombe pamoja na kila kitu walichonacho.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu hao ni wachunga mifugo, huchunga mifugo, wamekuja na makundi ya kondoo, mbuzi na ng’ombe pamoja na kila kitu walicho nacho.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watu hao ni wachungaji, maana wamekuwa watu wa kuchunga wanyama, nao wameleta kondoo zao, na ng'ombe zao, na yote waliyo nayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitamweleza kwamba nyinyi ni wachungaji kwani mmekuwa mkichunga mifugo, na kwamba mmewasili pamoja na mbuzi, kondoo, ng'ombe na mali yenu yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watu hawa ni wachungaji, kwani ni wenye makundi, nao mbuzi na kondoo wao na ng'ombe wao nayo yote, waliyokuwa nayo, wameyaleta huku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watu hao ni wachungaji, maana wamekuwa watu wa kuchunga wanyama, nao wameleta kondoo zao, na ng’ombe zao, na yote waliyo nayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitamwelezea kwamba ninyi ni wachungaji maana mumekuwa mukichunga nyama, na kwamba mumefika pamoja na mbuzi, kondoo, ngombe na mali yenu yote.